Kamati ya kudumu ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Huduma za Jamii imefanya ziara Mkoani Pwani kutembelea Viwanda vya Madawa ya Binadamu na chanjo kwa ajili ya Mifugo.
Wajumbe wa Kamati hiyo wakiongozwa na Mwenyekiti wao Mhe. Stanslaus Nyongo wamepokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe Abubakar Kunenge leo Februari 19,2024 ambaye amewaeleza kuwa uwekezaji mkubwa wa viwanda umefanyika ikiwemo kwenye viwanda vya Madawa na kuwa Mkoa una jumla ya viwanda 1533 vikiwemo viwanda 122 vikubwa.
Ameeleza kuwa maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya viwanda likiwemo la Zegereni ambako kuna viwanda vya madawa tayari Serikali imepeleka miundombinu ya Barabara ya lami ambapo takribani shilingi Bilioni 16.6 zimetumika kwenye ujenzi wa Barabara hiyo na takriban shilingi Bilioni 3.39 zimetumika kukamilisha mradi wa Maji kwenye eneo hilo.
Kamati hiyo imetembelea Viwanda vya madawa vya kampuni ya Kairuki Pharmaceutical co Ltd, Katwaza Pharmacy na kiwanda cha Chanjo za Mifugo Hester Biosciences Tanzania Ltd.
Naye Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Stanslaus Nyongo ameeleza kuwa amefika Mkoani humo kuangalia Uwekezaji uliofanyika kwenye sekta ya Afya na kuwa Kamati hiyo iliishauri Serikali kuwekeza ba sasa wamekuja kuona hali ilivyo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.