Kamati hiyo ya kudumu ya Bunge ya Mazingira na Maji imefanya ziara ya siku moja Wilayani Rufiji na Kutembelea maeneo yaliyoathirika na Mvua za Elnino na Kuwapa pole wananachi.
Akizungumza kwenye Mkutano wa Wananchi wa Kata ya Muhoro Kunenge amewaeleza Kamati jitihada za Serikali zilizofanyika katika kunusuru maisha ya Wananchi hao wakati wa kipindi cha athari hizo.
Ameeleza Wilaya za Kibiti na Rufiji zilikumbwa na Athari za mafuriko ya mvua za Elnino na Kimbunga Hidaya kwa Wilaya ya Mafia.
Ameeleza kuwa Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan amefanya jitihada kubwa katika kutatua kero changamoto kubwa iliyotupata.
Mwenyekit wa Kamati Mhe Jackson Kiswaga ameipongeza Serikali kwa ujumla Kwa jitihada zote zilizofanyika na kwamba wamefika kujionea hali ilivyo na kuwapa pole wananchi. Ameeleza kuwa Mhe Rais anawapenda na kwamba ameleta misaada mingi ikiwemo ya kwake yeye binafsi.
Amewataka wananchi kupokea na kuzingatia ushauri wa kitaalamu na kuyafanyia kazi tafiti za kisayansi. Ameeleza eneo hilo la Muhoro Rufiji ni eneo la mkondo wa maji na kwamba Serikali imetafuta eneo salama kwa wananchi. Amewataka wananchi kuchukua hatua za haraka na kuzingatia tahadhari za mazingira zilizotolewa.
Ziara hiyo imehudhuriw na Mhe Khamis Hamzq Khamis Naibu waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira,Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Eng Luhemeja.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.