Kanda ya Mashariki ni kanda kubwa katika kukuza uchumi ba Sekta ya Kilimo, Ufugaji na uvuvu, kauli hiyo imetolewa na Waziri mkuu Mstaafu mhe. Mizengo Pinda wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya Nane Nane Kanda ya Mashariki yaliyofanyika katika Viwanja vya Nane nane Mkoani Morogoro
Aidha ameeleza kuwa hakuna zao ambalo halikubali katika Kanda hiyo kwa kuwa Kanda hiyo ina hali ya hewa tofauti tofauti. Amepongeza Mkoa wa Pwani kwa kuwa kinara katika Ujenzi wa Uchumi wa Viwanda Nchini.
Pinda alisema kauli mbiu ya Maonesho hayo ni Vijana na Wanawake ni Msingi wa mifumo endelevu ya Chakula. Ameeleza hilo kwa kuwa Wanawake ni jicho muhimu katika Chakula ikiwemo lishe kwa watoto. Vijana ni kwa sababu lazima waanze jitihada leo ikiwemo kukabiliana na Changamoto za kilimo na mfumo wake uwe wa mashamba makubwa. Pia amesema kuwa Takwimu za sensa ya 2022 zinaonesha Kanda ya Mashariki ina vijana asilimia 36 juu ya asilimia ya Taifa ambayo ni asilimia 34.
Katika hatua nyingine Pinda ametoa rai kwa Viongozi wa Mikoa ya Kanda ya Mashariki Kujipanga na programu ya Mradi wa Build Better Tomorrow. Kwa kuanisha mashamba hayo pale ambapo vijana watajitokeza kutaka kujiendeleza katika sekta hizo.
Nae Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge akitoa salaam za Mkoa na Kanda ya Mashariki amesema kuwa Matarajio ya Mkoa ni kuhakisha matarajio na matamanio ya Mhe Rais yanafikiwa na yeyote mwenye shaka na jitihada na kazi za Mhe Rais aje kuona na kushuhudia Mkoani Pwani na kanda ya Mashariki.
Kunenge ameeleza, Mkoa Pwani unaendelea kuhakisha Vipaumbele vya Mkoa wa Pwani ni sahihi na Vipaumbele hivyo ni Vipaumbele vya Mhe Rais na juhudi za Mkoa ni kuanzisha mazao mapya ikiwemo Michikichi na Mpunga.
Amefafanua zaid kuwa mazao ya Ufuta na Korosho yameendelea kufanya vizur Mkoa wa Pwani ikiwemo kiwango cha ubora wa Daraja la kwanza kufikiq asilimia 92 kwa msimu uliopita dhamira ya Mkoa na Kanda ya Mashariki ni kuona tunachangia katika kulisha Tanzania na Dunia nzima.
Ameeleza kuwa washiriki wa maonesho hayo kwa mwaka 2023 wameongezeka kutoka watu 477 hadi 589 ikiwa ni ongezeko la asilimia 22.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.