Mkuu wa wilaya ya Kibiti Mhe. Kanali Joseph Samwel Kolombo amesema Wilaya hiyo imejipanga kutimiza malengo waliyowekewa na serikali ya uzalishaji wa korosho kufikia tani 14,000 kwa mwaka huu wa 2025.
Amesema tayari serikali imeandaa pembejeo za kutosha kwa ajili ya kuwasambazia wakulima wa zao hilo wilayani humo.
Aidha katika taarifa yake hiyo aliyoitoa leo Agosti 27, 2025 Ofisini kwake alipotembelewa na Katibu Tawala Mkoa wa Pwani aliyefika katika Wilaya hiyo kwa ziara ya siku moja kuzungumza na watumishi, kutembelea na kukagua Miardi ya maendeleo, iliyogusia maeneo mengi ya kimaendeleo, Mhe. Kolombo aliishukuru serikali ya awamu ya nne kwa kutenga pesa zaidi ya shilingi bilioni 43 ambazo zimetumika katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo Elimu, Afya, Nishati na Kilimo hata kusogeza zaidi huduma za kijamii kwa wananchi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.