Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhe. Abubakar Kunenge, leo amekutana na wawakilishi wa kampuni ya Rothly kutoka China na Marekani, wakiongozwa na Bwana Justice Kaundama, mmiliki wa kampuni ya usafirishaji ya Shamwaa Afrika kutoka China, kwa mazungumzo kuhusu fursa za uwekezaji katika mkoa huo.
Katika mazungumzo hayo, Mhe. Kunenge alitoa hakikisho la mazingira bora kwa wawekezaji, akitaja miundombinu madhubuti, upatikanaji wa umeme wa uhakika, barabara bora, nguvu kazi ya kutosha, masoko thabiti kwa bidhaa, na maji safi na salama kama vivutio muhimu kwa uwekezaji wa kimataifa.
“Pwani ni eneo lenye fursa nyingi na mazingira bora kwa uwekezaji.
Tunakaribisha wawekezaji kutoka ndani na nje ya nchi kushirikiana nasi katika kukuza maendeleo ya kiuchumi,” alisema Kunenge.
Mazungumzo haya yanadhihirisha jitihada za Mkoa wa Pwani kuvutia uwekezaji wa kimataifa ili kuchochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika mkoa huo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.