Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge amezielekeza Halmashauri za Mkoa huo kuibua na kuendeleza vipaji vya michezo miongoni mwa wanafunzi wa shule za Msingi na Sekondari.
Katika salaam zake za zilizowasilishwa kwa niaba yake na Katibu Tawala wa Mkoa huo ambaye pia ni Skauti Mkuu wa Tanzania Rashid Mchatta wakati wa ufunguzi wa mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma kwa Shule za Msingi Tanzania (UMITASHUMTA) yaliyofanyika kwenye viwanja vya Shirika la Elimu Kibaha (KEC) leo Mei 31, 2024, mkuu huyo wa Mkoa amesisitiza kuwa hilo linawezekana iwapo Halamashauri zitatenga, kutoa na kutumia fedha kwa ajili ya shughuli hiyo.
"Michezo ni ajira pia ni afya ambapo baadhi ya watu wamefanikiwa duniani kupitia michezo hivyo lazima kuwawekea mazingira mazuri vijana, hivyo ili kufanikisha kuibua na kuendeleza vipaji vya watoto walioko mashuleni, ni vema Halmashauri zikatenga fedha ili ziweze kufanikisha michezo ya UMITASHUMTA na ya Umoja wa Michezo kwa Shule za Sekondari Tanzania (UMISSETA)," amesema.
Jumla ya wanamichezo 516 katika fani mbalimbali na walimu 17 wamechaguliwa kushiriki katika mashindano ya UMITASHUMTA Taifa yatarajiwa kufanyika Mkoani Tabora Mwezi Juni Mwaka huu.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.