Mamia ya wananchi kutoka mikoa ya Pwani, Dar es Salaam na maeneo jirani wanatarajiwa kushiriki tamasha kubwa la Utalii lijulikanalo kama "Mafia Festival," litakalofanyika Septemba 28 hadi 30 katika fukwe za Utende zilizopo wilayani Mafia mkoa wa Pwani.
Tamasha hilo litahusisha shughuli mbalimbali ikiwemo kujadili fursa za uchumi wa bluu zinazopatikana kupitia bahari ya Hindi, kilimo cha Mwani na ufugaji wa Samaki.
Mkuu wa Wilaya ya Mafia, Zephania Sumaye ametoa kauli hiyo leo Septemba 15, 2023, alipofika kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa na kufanya mahojiano na mwandishi wa habari hii katika ofisi za Mkuu wa mkoa wa Pwani kuhusu maandalizi ya tamasha hilo ambalo litakuwa la kipekee kutokana na eneo hilo kuwa na vivutio vya kipekee.
“Mafia iko tayari kupokea wageni kwa ajili ya maonesho haya, matumaini yetu ni kuwa wananchi watafurahia na kujifunza mambo mengi yanayopatikana kama vile utalii wa boti, jukwaa la biashara ambalo litajadili fursa za uchumi wa bluu ili kuinua pato la mwananchi na taifa sambamba na burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali nchini,” amesema Sumaye
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.