Halmashauri ya Wilaya ya Mafia imetakiwa kufanya tathmini ya kiasi inachochangia kwenye pato la taifa (GDP) ili kuona kama inaufanisi katika kuchangia maendeleo ya wananchi.
Maelekezo hayo yametolewa leo Juni 24, 2023 na Mkuu wa Wilaya hiyo Zephania Sumaye aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge kwenye kikao cha Baraza la madiwani wa halmashauri ya Wilaya hiyo maalum kilichoketi kujadili hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali - CAG kwa mwaka wa fedha 2022/23.
Katika maelezo hayo, Sumaye ameipongeza halmashauri hiyo kwa kufanya vizuri katika kufuta na kupunguza hoja kwani hadi sasa imebakiwa na hoja 13 tu kutoka kwenye jumla ya hoja 51 ambapo 38 zimefungwa, zilizobaki nyingi ni zilizo nje ya utekelezaji wao wa moja kwa moja tofauti na halmashauri zingine za mkoa huo ambazo pamoja na kupunguza, bado zina idadi kubwa.
Kuhusu kuongeza mapato ya ndani ya halmashauri hiyo, DC Sumaye amesema ni wajibu wa halmashauri hiyo kubuni vyanzo vipya na kuboresha vilivyopo bila kumkamua mwananchi.
"Tumepanga kufanya operesheni ya kukamata walanguzi na kuzuia magendo ili tuweze kuwa na makusanyo mazuri kwani ninatamani ndani ya kila miezi sita ya mwanzo katika kila mwaka wa fedha tuwe tumefikia au kuvuka lengo la makusanyo ya mapato ya ndani, nipo tayari kutoa kila aina ya msaada na ushirikiano kufanikisha hilo," amesema Sumaye.
Akifafanua baadhi ya hatua wanazopanga kutekeleza ili kukuza uchumi na kuongeza mapato ya ndani ya halmashauri hiyo, Sumaye amesema kuwa wameandaa tamasha kubwa la utalii lenye lengo la kuongeza idadi kubwa ya watalii katika kisiwa hicho.
Naye Katibu Tawala Msaidizi Ufuatiliaji, Usimamizi na Ukaguzi Nsajigwa George aliyemwakilisha Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani kwenye kikao hicho, mbali na kuipongeza halmashauri hiyo kupata hati safi, pia ameiasa kuendelea kupambana zaidi na kuwa wafanye hivyo kwa ajili ya maslahi ya wananchi.
Kuhusu upungufu wa watumishi, Nsajigwa amesema kuwa Katibu Tawala Mkoa anaitambua changamoto hiyo hasa kwa mafia na tayari ameshaitisha ikama ili taratibu za kufanya msawazo ziendelee.
"Suala sio tu kukuletea watumishi, ni kwa namna gani mnawabakiza hapa ili waongeze juhudi, kasi ubunifu na mtambue kuwa kazi zako ndizo zinazokubeba, ongezeni bidii na juhudi na wala msikate tamaa wala kurudi nyuma katika kutekeleza wajibu wenu kwa idadi yenu hiyo hiyo," amesema Nsajigwa.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Juma Salum ametoa rai kwa madiwani kusimamia Udhibiti wa uvuvi haramu akisema "tusioneane aibu, ukishakuwa
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.