Mhe Salvador Valdes Mesa Makamu wa Rais wa Cuba January 24, 2024 ametembelea kiwanda cha Viwadudu Tanzania Biotech Products Ltd kilichopo Kibaha
Akimkaribisha Mkoani Pwani Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe Abubakar Kunenge Amesema kuwa pamoja na kuwa na ratiba ngumu ameweza kufika kibaha.
Amempongeza Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa juhudi zake za kuendelea kuvutia uwekezaji. Ameendelea kuwakaribisha wawekezaji kutoka Nchini Cuba Kuja kuwekeza Nchin Tanzania na kuwahakikishia kuwa watapata sapoti ya Serikali katika Nyanja zote katika uwekezaji wao.
Naye Makamu wa Rais wa Cuba akisalimia hadhira iliyokusanyika kiwandani hapo, amesema kuwa yupo katika ziara ya kiserikali Lakin pamoja na ratiba ngumu aliyonayo hawakutaka kuondoka nchini bila kutembelea kiwanda hicho. Ameeleza kuwa uhusiano wa Tanzania na Cuba ni wa muda mrefu na
Ameongeza kuwa anayo furaha kutembelea kiwanda hicho kwa mara ya pili mara ya kwanza ilikuwa 2016. Kipindi hicho kilikuwa ni ujenzi. Lengo la Kiwanda hicho ni kupamba na kutokomeza malaria katika Nchi zetu. Amesema kuwa kwa sasa tunahaja ya kukipnua na kuongeza uzalishaji ili kiwanda kizalishe katika kiwango cha juu.
Makamu wa Rais huyo ameishukuru serikal ya Tanzania na kuahidi kuwa wataendelea kutoa msaada wa kiufundi na kitaalam ili kufanikisha zaidi uzalishaji wa madawa hayo.
Makamu huyo wa Rais ameeleza kuwa kiwanda hicho kimetoa ajira zaid 100, na kusema kuwa kiwanda hicho ni mhumu kwa uchumi wa nchi zetu na majirani zetu.Kwani kupitia madawa hayo tutatokomezaa malaria na magonjwa yanayoenezwa na wadudu.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.