Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Mizengo Kayanza Pinda, amesema Maonesho ya Nanenane Kanda ya Mashariki ya mwaka 2025 ni ya kipekee na yamepiga hatua kubwa katika ufanisi. Ametoa wito kwa mamlaka husika kuweka alama za ubora kwenye bidhaa zinazozalishwa na halmashauri pamoja na wajasiriamali ili kuongeza thamani na ushindani wa soko.
Akifungua rasmi maonesho hayo Agosti 2, 2025, katika Viwanja vya Julius Kambarage Nyerere mkoani Morogoro, Mhe. Pinda alisema bidhaa nyingi zimefungashwa kwa viwango vya kimataifa, na kuongeza kuwa hatua zaidi zinahitajika ili kuvutia masoko mapya.
Pia alimpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa sera bora zinazokuza sekta za kilimo, mifugo na uvuvi.
Mhe. Pinda alihimiza umuhimu wa kutumia kikamilifu fursa zilizopo katika Kanda ya Mashariki na kushauri kufanyika kwa kikao cha tathmini kila baada ya maonesho ili kujadili mafanikio, changamoto na mikakati ya kuboresha maonesho yajayo. Maonesho haya yanajumuisha mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Morogoro na Tanga, chini ya kaulimbiu: “Chagua Viongozi Bora kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi.”
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.