Mwenge wa Uhuru umeanza mbio zake Mkoani Pwani ambapo unatarajiwa kutembelea miradi 81 yenye thamani ya sh.bil 225,132,007, 721(Billioni miambili ishirini na tano, milion miamoja thelathini na mbili na elfu saba miasaba ishirini na moja.
Akipokea Mwenge huo kutoka Mkoa wa Dar es Salaam, Mkuu wa Mkoa wa Pwani ,Mhe. Mhandisi Evarist Ndikilo, alisema kati ya miradi hiyo ,25 itawekewa mawe ya msingi ,miradi 27 itazinduliwa, miradi 4 itafunguliwa na miradi 25 itakaguliwa.
Miradi hiyo yote imechangiwa kwa pamoja na Wananchi, Serikali Kuu, Halmashauri na Wahisani wa ndani na nje.
Mhandisi Ndikilo alisema, Mkoa unatekeleza kwa vitendo Ujumbe wa Mwenge “Shiriki kukuza uchumi wa viwanda kwa maendeleo ya nchi yetu” ambapo kwa sasa Mkoa una viwanda 264. “Kati ya hivyo viwanda vikubwa ni 84 na vidogo 176 na kila Halmashauri imetenga maeneo kwa ajili ya uwekezaji na kuna fursa nyingi sana za uwekezaji kwenye Mkoa wetu na tumeweka mazingira mazuri kwa wawekezaji,” alisema Mhandisi Ndikilo.
Alieleza mbali ya kuhimiza uwekezaji wa viwanda pia wanapambana na maradhi ya UKIMWI na Malaria pamoja na madawa ya kulevya na rushwa.
Mwenge huo umeanza mbio zake Wilayani Mafia June 1 na june 2,utakuwa Wilayani Kibiti.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.