Katibu Tawala Mkoa wa Pwani Rashid Mchatta amewaelekeza watendaji wanaohusika na Mpango wa kunusuru kaya masikini unaotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kuhakikisha wanaonyesha hali halisi ya kile kinachofanyika kwenye maeneo yaliyolengwa.
Mchatta ametoa maelekezo hayo June 26 alipokuwa akifungua kikao kazi kilichofanyika Mjini Kibaha ambacho kilikuwa kinajadili taarifa ya utekelezaji wa mpango huo kwa mkoa wa Pwani.
Katibu Tawala huyo amesema tathmini ya utekelezaji wa mpango wa TASAF inatakiwa kuonekana na kwenye maeneo yanayotekelezwa Mpango huo kwa kuona mabadiliko kwa walengwa.
"Mkitembelea kwenye maeneo ya mpango mnatakiwa kuonyesha nini kimefanyika Ili maeneo mengine waone namna Mpango huo ulivyotekelezeka na kuleta matokeo chanya kwa walengwa,"amesema.
Mkurugenzi wa Uratibu wa TASAF Haika Shayo ambaye alimwakilisha Mkurugenzi wa TASAF amesema wamefanya ziarq katika Mkoa wa Pwani kuo kuona utekelezaji wa mpango kwa walengwa wakiambatana na wadau wa maendeleo
Amesema Ili uendelea kuwainua wanufaika katika shughuli zao za kiuchumi ni vema wakaunganishwa na Shirika la viwanda vidogovidogo iwe tlrahisi kwao kutangaza bidhaa zao na kupata wanunuzi.
Mratibu wa wa TASAF Mkoa wa Pwani Roseline Kimaro amesema kupitia Mpango huo wanufaika wamekuwa na mabadiliko ya kiuchumi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.