Katibu Tawala Mkoa wa Pwani (RAS),Rashid Mchatta amewaasa Maafisa elimu Mkoani humo, kuhakikisha wanasimamia na kutekeleza viashiria vya utendaji walivyojiwekea.
Rai hiyo ameitoa leo Juni 1, 2023 wakati akifungua kikao kazi cha tathmini ya utekelezaji wa kuboresha elimu ngazi ya Mkoa, kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano Halmashauri ya Mji Kibaha.
Mchatta alisema ,kikao hiki ni cha pili kufuatia kikao cha REM kufanyika Machi 21, 2023 ambapo baadhi ya maazimio yalipitishwa ikiwa ni kuhakikisha wanafunzi wa darasa la pili hadi la Saba wanamudu stadi za KKK ifikapo Mei 30 2023,kutokomeza Utoro wa rejareja kwa wanafunzi wa shule za Msingi na Sekondari.
Pia kuweka mikakati ya kuhakikisha kuwa wanafunzi waliofeli na kukariri darasa la nne na kidato cha pili wanafaulu na kupandisha ufaulu wa wanafunzi wa darasa la Saba, la nne , kidato cha nne na cha Sita.
Vilevile, amesema bado utekelezaji wa mikakati hiyo hauridhishi, mathalan imebainika kuwa wanafunzi wasiomudu stadi za KKK bado wapo ingawa kwenye kikao cha REM kiliazimia wanafunzi hao waweze kumudu stadi hizo ifikapo Mei 30 2023.
"Utekelezaji huu unatutathmini sisi kama viongozi, hatua stahiki zitachukuliwa kufuatia mikataba iliyosainiwa";Hivyo natoa rai ya kutekeleza majukumu yenu kama mikataba inavyoeleze" alisisitiza Mchatta.
Hiki ni kikao kazi cha pili ambacho kimehusisha Maafisa Elimu wa Msingi na Sekondari kutoka ngazi ya Mkoa, Wilaya, Kata zote zilizopo Mkoa wa Pwani.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.