Na: Nasra Mondwe
Katibu Tawala Mkoa wa Pwani Mhandisi Mwanasha Tumbo amewataka watumishi wote wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani,Kutoa huduma nzuri kwa Wananchi ambao ni wateja wote wa ndani na Nje ya Ofisi hiyo.
Amesema kwa kufanya hivyo watakuwa wamemsaidia Mhe. Rais ambaye tegemeo lake kubwa ni kuona Serikali za Mikoa zinasimamia majukumu yote na kushughulikia Malalamiko ya Wananchi. Ametoa rai hiyo Juni 3, 2021 wakati akizungumza na Watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwenye hafla fupi ya Makabidhiano iliyofanyika Ofisini hapo.
Mhandisi Tumbo amewaeleza Watumishi hao kuwa katika kutoa huduma kwa Wanachi wanapaswa kujali Wanachi wanofika Ofisini hapo kutafuta huduma kwa kuwahudumia kwa wakati na kutumia Lugha nzuri katika kuhudumia. Amewaeleza Watumishi hao kuwa katika kutekeleza Majukumu yao yote wafahamu kuwa wanatekeleza Ilani ya Chama, Chama Cha Mapinduzi ambao ndiyo wenye Serikali.
"Watumishi ni sawa na Wauza Duka na Wenye Duka ni Chama Chama cha Mapinduzi, Watumishi tukiwa wauzaji wa Duka hili tuuze Vizuri kwa makini na kwa uaminifu" alisema Tumbo, Amewataka kutoa Ushirikiano kwa Chama cha Mapinduzi pale Chama kinapohoji utekelezaji wa majukumu mbali mbali kwa kuwa wanatekeleza ilani yake.
Amesisitiza kufanya kazi kwa weledi na kuzingatia sheria na kanuni za utumishi wa umma, amewataka watumishi hao kumpa ushirikiano wa kutosha katika utendaji wa kazi na kuhakikisha wanawahi kufika kazini na kufanya majukumu yao,
Naye, Katibu Tawala aliyemaliza Muda Wake Dr. Delphine Magere amewashukuru Watumishi wa Sekretarieti ya Mkoa huo kwa kumpa ushirikiano katika kipindi chote alichokuwa kazini na amewataka watumishi hao kumpa Mhandisi Tumbo ushirikiano.
“Nimekaa na nyie kwa muda wa Mwaka mmoja na nawashukuru kwa ushirikiano mlionipa katika kipindi chote tulichokuwa pamoja, hivyo nawasihi kuwa ushirikiano mliokuwa mkinipa mimi nawaonba mumpatie pia Mhandisi Tumbo ili kuhakikisha Mkoa wa Pwani Unasonga mbele katika nyanja zote”alisema Dkt Magere.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.