Na .Nasra Mondwe
Katiubu Tawala wa mkoa wa Pwani Mhandisi Mwanasha Tumbo amefungua mashindano ya umoja wa michezo wa shule za Sekondari –UMISETA – na kuzielekeza halmashauri zote za Mkoa huo kuwapa fursa maafisa michezo pamoja na maafisa Utamaduni kutumia taalamuma zao kuendeleza michezo mkoani humo.
Akifungua mashindano hayo kwa niaba ya katibu Tawala hiyo ,Afisa Elimu Mkoa wa PWANI mwalimu Hildegard Makundi zungumza katika mashindano hayo yanayofanyika katika viwanja vya Shule ya Sekondari ya Kibaha Mhandisi Tumbo amesema hali hiyo itawasaidiamaafisa hao kutambua na kuwaibua vijana wengi ndani ya Mkoa huo ambao wanavipaji vya michezo ambavyo vikikuzwa vitatoa wachezaji bora ambao wataoletea sifa Mkoa huo
Amezitaka halmashauri hizo pia kuwaendeleza waalimu wa michezo kwa kuwapeleka katika vyuo vinavyofundisha michezo ikiwa ni pamoja na chuo cha maendeleo ya michezo Malya na taasisi ya sanaa na michezo Bagamoyo- Tasuba.
Katika salamu zake katibu Tawala huyo amewataka waamuzi wa mashindano hayo kutoa uamuzi wa haki bila upendeleo.
Kwa upande wake Ofisa Utamaduni wa Mkoa wa Pwani Janeth Kaminyoge amesema mashindano hayo yanajumla ya wanamichezo 703 kutoka katika hal,mashauri zote za mkoah huo .
Mashindano hayo ambayo yameafanyika katika viwanja vya Shirika la Elimu Kibaha yanajumuisha kichezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu, mpira wa mikono,(netball),mpira wa wavu,mpira wa meza, riadha na mpira wa kikapu.
Amesema baada ya mashindano hayo itachaguliwa timu ya mkoa itakayokwenda kuuwakilisha mkoa huo katika mashindano ya kitaifa yatakayofanyika mkoani Mtwara kuanzia tarehe 26 mwezi huu hadi tarehe 2 mwezi julai mwaka huu.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.