Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhe. Aboubakar Kunenge, ametoa wito wa kuhakikisha miradi ya barabara inazingatia mahitaji halisi ya wananchi, kama alivyoelekeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Akizungumza katika kikao cha Bodi ya Barabara cha mwaka wa fedha 2024/2025 kilichofanyika Decemba 4,2024, Kunenge alisisitiza kuwa timu maalum iundwe ili kuorodhesha vipaumbele vya miradi kulingana na changamoto zinazowakabili wananchi.
Alieleza kuwa utekelezaji wa miradi unapaswa kuanza na vipaumbele muhimu zaidi na kuendelea kwa mpangilio huo.
“Tunahitaji kuhakikisha miradi inatekelezwa kwa kufuata mahitaji halisi ya wananchi.
Tukianza na kipaumbele cha mwisho badala ya cha kwanza, tunakuwa hatujajibu changamoto za msingi za jamii,” alisema Kunenge.
Aidha, alisisitiza uwajibikaji wa viongozi katika usimamizi wa fedha za serikali, akihimiza matumizi mazuri yanayolenga kuleta matokeo yanayoonekana katika miundombinu ya barabara, usafiri, na usafirishaji.
Kwa kusimamia vipaumbele hivi, mkoa wa Pwani unalenga kuboresha huduma za usafiri na kuimarisha maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa wananchi wake.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.