Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge, leo Mei 24 amemkabidhi Mwenge wa Uhuru 2023 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila , ambapo alisema Mwenge wa Uhuru 2023 umepitia jumla ya Miradi 99 yenye Thamani ya Trilion 4.4, umbali wa kilometa 1000 katika Wilaya Saba za Mkoa na Halmashauri 9, ambapo kati ya Miradi hiyo miradi 9 ilifunguliwa,15 ilizinduliwa,20 iliwekewa mawe ya msingi na 55 ilikaguliwa.
Kunenge amefafanua ,Miradi yote 99 iliyopitiwa na Mwenge wa Uhuru 2023 haikuwa na Dosari na yote imekubaliwa.
Ameeleza kuwa mbio za Mwenge wa Uhuru 2023 yenye kauli mbiu isemayo "okoa vyanzo vya maji kwa ustawi wa Viumbe hai" itasaidia kulinda na kutunza mazingira, kufanya mkoa kuendelea kuwa wa kijani.
Kunenge amesema ,katika kuunga mkono jitihada za Serikali kutunza mazingira umeweka mkakati wa kuhamasisha upandaji wa miti ambapo hadi kufikia mwezi April 2023 jumla ya miti 7,772,549 sawa na asilimia 57.7 ya lengo la kupanda miti Milion 13 kwa mwaka huu na wakati wa mbio za Mwenge za Uhuru jumla ya miti 5,917 ilipandwa .
Pia katika mapambano dhidi ya Rushwa Mkoa ulichukua hatua zifuatazo" kuanzia Julai 2022 hadi April 2025 TAKUKURU imeendesha jumla ya kesi 35 na kati ya hizo kesi 7 zilitolewa maamuzi na 28 zinaendelea.
Mkoa wa Pwani ulipokea Mwenge wa Uhuru Mei 15 ukitokea Mkoani Morogoro ambao ulikimbizwa katika Halmashauri zote 9 za Mkoa kisha kuukabidhi Mkoa wa Dar es Salaam.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.