Hayo yamebainishwa Mei 27 2020 Kwenye Kikao cha Wadau wa Ufuta Mkoani Pwani.
Akifungua Kikao hicho Mhe. Mhandisi Evarist Ndikilo Mkuu wa Mkoa wa Pwani amesema
"Ufuta ni Uchumi wa Mkoa wetu na Taifa kwa Ujumla hivyo tumekutana kuweka mipango ya kufanikisha mauzo ya Ufuta kupitia mfumo wa Stakabadhi Ghalani katika minada itakayo fanyika katikati ya Mwezi Juni".
Mhandisi Ndikilo ameeleza kuwa Mkoa wa Pwani ni Mkoa unaozalisha zao la Ufuta kwa wingi Nchini. akitolea mfano wa Msimu wa mwaka 2019/2020 amesema jumla ya Tani 7,327 zenye thamani ya shilingi Bilioni 19.35 zilikusanywa na kuuzwa kupitia Maghala ya AMCOS.
Aidha aliendelea kusema kuwa Matarajio kwa Msimu wa Mwaka huu 2020/2021 unatarajiwa kuwa ni Tani 13.25 mara mbili ya mwaka jana.
Pia amesisitiza kuwa ni wajibu wao kama Serikali ya Mkoa kuhakikisha zao hilo linamnufaisha Mkulima. “hawa ni wakulima wanyonge ambao Serikali inataka tuwalinde kwa nguvu zetu zote “alisema Ndikilo.
Akizungumzia Mfumo utakao tumika Mhandisi Ndikilo ameeleza kuwa kwa msimu huu Minada itafanyika kwa njia Kielectroniki kupitia Soko la bidhaa Tanzania (Tanzania Mercantile Exchange- TMX) na kwa njia ya Sanduku. litaanza Sanduku kwa wanunuzi kuweka bei na baadae litafungwa wataendelea na mtandao mwisho watalinganisha bei kupata bei nzuri inayomnufaisha Mkulima.
Akielezea Mfumo huo alisema, Wanachama na wakulima watapeleka ufuta kwenye Maghala ya vyama vya ushirika vya msingi ambavyo vitapeleka ufuta kwenye maghala makuu yaliyosajiliwa na Bodi ya Leseni za Maghala Tanzania, baadaye maghala makuu yatapeleka taarifa za ufuta uliopokelewa TMX ambayo itaratibu minada hiyo .
Katika hatua nyingine alielekeza wakulima walipwe katika akaunti zao na wakala wa vipimo wasimamie ubora wa mizani ili wakulima wasipunjwe .
Hata hivyo ,aliwaelekeza viongozi na watendaji wa vyama vya ushirika wahakikishe vifungashio vya ufuta ghafi vinapatikana kwa wakati kwa wakulima.
Mara baada ya Mnada kufanyika malipo yafanyike haraka kwa Wakulima na wanunuzi wajitahidi kutoa mzigo kwa haraka kwenye maghala ili kutoa nafasi kwa mzigo mwingine unaofuata.
Mhandisi Ndikilo alitoa rai kwa wadau wote wanaohusika kutimiza wajibu wao kikamilifu ili kuwapa manufaa Wakulima kwenye zao la ufuta.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.