Ofisa Mipango na Uratibu Mkoani Pwani,Rukia Muwango ameeleza Mwaka wa fedha 2022/2023 mkoa huo umeidhinisha bajeti ya Bilioni 335.110.456.0 kati ya hizo ruzuku ya matumizi ya kawaida ni Bilioni 206.063.8 ,sh.80,568.2 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo na 48,478,338,000 za mapato ya ndani ya Halmashauri.
Alieleza bajeti ya mkoa wa Pwani kwa mwaka 2022/2023 imeongezeka kwa Bilioni 36,279,573,000 sawa na asilimia 12.14 ikilinganishwa na bajeti ya mwaka 2021/2022.
Hayo ameyaeleza lwakati wa kikao cha Kamti ya Ushauri ya Mkoa kilichofanyika leo January 5, 2023.
Rukia alifafanua , ongezeko hilo linatokana na ongezeko la mishahara kwa asilimia 19.38, matumizi mengine (oc) asilimia 21.82, fedha za ndani kwa ajili ya miradi ya maendeleo asilimia 9.44 na mapato ya ndani ya Halmashauri asilimia 23.33.
"Bajeti ya miradi ya maendeleo kwa fedha za nje imepungua kwa asilimia 24.86 ,kwa ujumla bajeti ya mkoa imekuwa ikiongezeka mwaka hadi mwaka.
Changamoto, alisema mkoa umepata changamoto kubwa ya kufanya uhamisho wa ndani na nje wa bajeti kwa fedha zilizopokelewa nje ya bajeti.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.