Mkoa wa Pwani ni miongoni mwa mikoa 26 inayotekeleza Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (TASAF), ukilenga kuboresha maisha ya kaya zenye uhitaji kwa kuwapatia ruzuku na fursa za ajira za muda.
Katika robo ya tatu ya mwaka wa fedha 2024/25 Dirisha la 22 la malipo kwa wanufaika limefunguliwa na linatarajiwa kufungwa ifikapo Februari 6, 2025. Mkoa umejipanga kusimamia na kuratibu zoezi la ulipaji wa ruzuku kwa kuhakikisha wanufaika wanapata fedha zao kwa wakati na kwa njia salama.
Mbali na ulipaji wa ruzuku, shughuli nyingine zinazotekelezwa ni utoaji wa elimu kuhusu matumizi ya nishati safi, Utekelzaji wa miradi ya ajira za muda (PWP), pamoja na miradi ya Miundombinu (T.I). Kwa mujibu wa takwimu, wanufaika 20,662 wanatarajiwa kupokea ruzuku, ambapo 6,459 watapokea kwa njia ya taslimu na 14,203 kwa njia ya mtandao.
Mkoa unaendelea na mikakati ya kuhakikisha wanufaika wote wanapokea ruzuku zao kwa njia ya mtandao ili kuongeza ufanisi na kuhakikisha fedha zinawafikia kwa wakati. Wataalamu wanaendelea kutoa elimu kwa wanufaika kuhusu matumizi ya mifumo ya kidijitali ili kurahisisha kupokea Malipo yao.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.