Serikali imesema ifikapo mwishoni mwa Mwezi Novemba Mwaka huu Ujenzi wa Mtambo wa kupoza Umeme katika Ktuo cha Chalinze utakuwa umekamilika na hivyo kuondoa kabisa chamgamoto ya Umeme nchini.
Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Dotto Biteko alipofamya ziara ya kutembelea na kukagua maendeleo ya Ujenzi wa Kituo cha kupoza Umeme Chalinze mkoani Pwani.
Amesema hadi sasa ujenzi wa Mtambo huo umefikia asilimia 84,3 na utakapokamilika ifikapo Desemba mwaka huu mtambo huo utaanza kupokea Umeme rasmi kutoka kwenye Bwawa la kufua Umeme la Julius Nyerere na kuingizwa katika Gridi ya Taifa kwani Ujenzi wa njia ya kusafirishia umeme kutoka kituo hicho hadi Bwawa la Mwl Nyerere ujenzi wake umefikia asilimia 99.
Dkt. Biteko ameaema, mtambo huo utakapoanza kupokea nishati hiyo, utasaidia nchi kupata Umeme wa kutosha kwa matumizi ya Viwanda na ya shughuli zingine za kijamii na akafafanua kuwa Mikoa ya Pwani na Dar es Salaam pekee inatumia nusu ya Mega Walt za Grid ya Taifa kwa matumizi hayo.
Amesema Serikali itahakikisha inatatua changamoto ya umeme nchini hatua kwa hatua ili kupunguza tatizo lililopo kwenye maeneo ambayo hayajapata nishati hiyo.
Mkurugenzi wa miradi wa Shirika la Umeme nchini - TANESCO Mhandisi Declan Mhaiki amesema, wanatarajia kuzalisha Umeme wa Mega Walt 2115 kutoka Bwawa la Julius Nyerere ambao utaunganishwa kwenye Kituo cha kupoza Umeme Chalinze na Grid ya Taifa.
Naibu Waziri Mkuu huyo amepongeza hatua ya Ujenzi ulipofikia na kupongeza vijana walioajiriwa katika Ujenzi wa kituo hicho akisema kuwa Serikali inathamini mchango wao katika ujenzi huo.
Kwa upande wake Meneja Msimamizi wa Kituo cha Kupoza Umeme Chalinze Newton Livingstone ameeleza kuwa baada ya Umeme kupozwa, utasafirishwa kwenda kwenye Grid za Taifa za Kinyerezi, Ubungo - Dar es Salaam na Morogoro.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge amesema kukamilika kwa Mradi huo hautakuwa na manufaa kwa.
Watanzania pekee bali hata nchi Jirani nao watanufaika na mradi huo ambao ameahidi utalindwa na kuwa katika mikono salama na kuwa uongozi wa Mkoa umekuwa karibu na kituo hicho kuangalia maendeleo ya mradi huo.
"Huu ni mradi mkubwa kwa ajili ya kupoozea umeme, hivyo Halmashauri pangeni eneo linalozunguka mradi huu ili liwe na tija zaidi," amesema Kunenge.
Kunenge alieleza vijana walioajiriwa wamepata ujuzi na ujira.
"Umeme utapoozwa kutoka Kv 220 Kuja 132 na kuunganisha kwenye gridi ya Taifa."alibainisha Kunenge.
Hivi karibuni, Rais samia alitoa miezi sita kuhakikisha changamoto ya umeme nchini ambayo kwa sasa inatajwa kusababishwa na upungufu wa maji katika vyanzo vya zamani vya kuzalisha umeme hapa nchini inamalizika.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.