Mwenge wa Uhuru mwaka 2025 umeanza rasmi mbio zake katika Wilaya ya Kisarawe, ambapo utahusisha ukaguzi wa miradi saba yenye thamani ya shilingi bilioni 1.197.
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Petro Magoti, alipokea mwenge huo na kueleza kuwa utapita umbali wa kilomita 195 ndani ya wilaya hiyo. Aidha, mwenge huo utaweka jiwe la msingi kwa mradi mmoja, kuzindua miradi mitatu, na kukagua miradi mingine mitatu.
Kuhusu ufadhili wa miradi hiyo, Magoti alisema kuwa kati ya shilingi bilioni 1.197 zilizotumika, shilingi milioni 599.331 zilitolewa na serikali kuu, milioni 178.1 zilitokana na mapato ya halmashauri, milioni 409.6 zilitolewa na wahisani, milioni 4.7 zilichangiwa kupitia nguvu za wananchi, huku shilingi milioni 5.6 zikichangiwa kupitia Mwenge wa Uhuru.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Selemani Jafo, alibainisha kuwa miradi hiyo itaboresha upatikanaji wa huduma za kijamii na kuinua uchumi wa wakazi wa Kisarawe.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.