Mkuu wa Wilaya ya Rufiji, Meja Edward Gowelle amepokea Mwenge wa Uhuru ukitokea wilayani Mkuranga, ambapo umepokea taarifa za miradi nane yenye thamani ya sh.milioni 757.9.
Kati ya miradi iliyokaguliwa ni pamoja na ghala lililopo katika kijiji cha Ikwiriri Kaskazini, bweni la wasichana shule ya Sekondari Ikwiriri, mradi wa mazingira katika shule ya msingi Shaurimoy , shule ya msingi Mgomba kijiji cha Mgomba yenye watoto wenye uhitaji maalum na kutembelea kikundi cha ushonaji Umwe Kati.
Hata hivyo, Mwenge wa Uhuru umeshindwa kutembelea na kukagua miradi miwili kati ya nane iliyokusudiwa ambayo ipo kata ya Utete kutokana na changamoto ya mvua kubwa zinazoendelea kunyesha na kusababisha uharibifu wa miundombinu ya barabara.
Miradi hiyo ni pamoja mradi wa barabara yenye kiwango cha lami yenye thamani ya sh.550M pamoja na kuweka jiwe la msingi katika mradi wa maji kijiji cha Nyandakatundu, Utete wenye thamani ya sh. 7.9M.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Godfrey Mzava, akipokea taarifa ya miradi hiyo, Mei 5,2024 katika eneo ambalo msafara umekomea, ametoa agizo la kuwasilishwa kwa nyaraka na picha mjongefu (video), Leo ili aweze kuzikagua
Awali akisoma taarifa ya mradi wa barabara Hamisi Muhidini Chikaula amesema,ujenzi ulianza kutekelezwa 11,agost 2022 na umekamilika April 10,2023 .
Anaeleza, mradi huo umegharimu kiasi cha sh.milioni 504.9 ikiwa ni fedha kutoka Serikali Kuu kupitia Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini( TARURA) wilayani Rufiji na utekelezaji wake umekamilika kwa asilimia 100.
"Lengo la mradi huo ni kuboresha miundombinu ya barabara ili kurahisisha masuala ya usafirishaji" anasema Chikaula.
Akielezea kuhusu mradi wa maji Kijiji cha Nyandakatundu ameeleza, ulianza kutekelezwa April 1,2023 na unatarajia kukamilika juni 1,2024 ambapo umegharimu kiasi cha sh. mil 7.9.
Chikaula amefafanua, hadi sasa utekelezaji wa mradi umefikia asilimia 95 na utakapokamilika utahudumia wananchi 1,119 wa Kitongoji cha Nyandakatundu.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.