Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Godfrey Mzava amehimiza wananchi wenye sifa, kujitokeza kuchukua fomu kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi wa Serikali za Vitongoji, Vijiji na Mitaa, mwaka2024.
Aidha amesisitiza kulinda amani na utulivu wakati wote wa chaguzi hizo.
Akitoa ujumbe wa Mwenge Mzava, wakati wa makabidhiano ya Mwenge Halmashauri ya Kibaha Mjini ukitokea Halmashauri ya wilaya Kibaha, viwanja vya shule ya msingi Visiga kata ya Visiga, aliwaasa wananchi kuwa mabalozi katika suala la kutunza amani na usalama wakati wote.
Vilevile aliwataka wananchi wakati wa chaguzi ukifika wajitokeze kwenye kampeni na kusikiliza ili kuwapima wagombea ilihali kazi ya kuchagua iwe rahisi.
Awali akipokea Mwenge wa Uhuru, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kibaha, Dkt. Rogers Shemwelekwa alifafanua, Miradi iliyotembelewa na kukaguliwa ni 15 yenye thamani ya bilioni 3.1.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.