Naibu Waziri wa Uchukuzi, Mheshimiwa David Mwakiposa Kihenzile, Januari 10, 2025, alitembelea ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani, ambako alikutana na Kaimu Mkuu wa Mkoa, Mheshimiwa Nickson Simon, ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kibaha. Katika kikao hicho, Mhe. Kihenzile alipokea taarifa kuhusu hali ya miundombinu ya viwanda na mifumo ya usafirishaji mkoani humo. Baada ya kikao, Naibu Waziri alitarajiwa kutembelea Mji wa Kwala.
Kwa upande wake, Mhe. Nickson Simon alielezea mafanikio makubwa yaliyopatikana katika Mkoa wa Pwani chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan. Alibainisha kuwa mkoa huo umeongeza viwanda vikubwa 78 na kufikisha jumla ya viwanda 1,553, mafanikio ambayo yamechangiwa na sera bora za uwekezaji zilizowekwa na serikali.
“Mkoa wa Pwani tuna viwanda vingi vikubwa na vidogo, vikiwemo vya madawa, njano, jenereta, saruji, na tailizi, ambapo baadhi ya bidhaa zake zinasafirishwa nje ya nchi. Mafanikio haya yanatokana na sera nzuri ya serikali yetu,” alisema Mhe. Nickson Simon.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.