Wamiliki wa Viwanda Mkoani Pwani waaswa kuzalisha bidhaa kwa kutumia vipimo vinavyostahiki ili kuzalisha bidhaa bora zenye viwango na kuleta ushindani kwenye masoko ya ndani na nje ya Tanzania.
Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo wakati akifungua semina iliyoambatana na maadhimisho ya siku ya vipimo Duniani .
Mhandisi Ndikilo amesema kuwa, Serikali kupitia taasisi zenye dhamana ya kushughulika na vipimo wamejipanga kuhakikisha kila mfanyabiashara anayezalisha bidhaa yake nchini atumie vipimo sahihi kwa ajili ya kupata ubora kwa matumizi ya wananchi.
“Vipimo ni kiungo muhimu sana kwa maendeleo ya viwanda ,biashara,Afya,ujenzi , Elimu na taasisi za kiutafiti wa kisayansi” alisema Ndikilo.
Aidha, Mhandisi Ndikilo amesema kwamba kutokana na utitiri wa viwanda uliopo Mkoani hapa ,amelitaka shirika la Viwango liendelee kutoa elimu kwa wenye viwanda ili kuondoa tatizo la kuzalisha bidhaa zisizo na ubora .
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Upimaji wa Ugezi (Meterology) kutoka shirika la Viwango Tanzania (TBS) Mary Meela amesema ,wenye Viwanda Mkoani Pwani bado havijachangamkia masuala ya ugezi ndio sababu shirika kupitia maabara ya ugezi imeamua kufunga safari kufanya maadhimisho Mkoani Hapa.
Maadhimisho ya Siku ya Vipimo duniani mwaka huu yameadhimishwa June 22 ambapo yameambatana na kauli mbiu isemayo “Muendelezo wa mabadiliko ya vizio vya Kimataifa”.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.