Wazazi Mkoani Pwani wameonywa na kuacha mara moja tabia ya kuwakataza watoto kwenda shule na kuwashawishi watoto hao kufanya vibaya kwenye mitihani yao ya kumaliza darasa la saba na kidato cha nne kushiriki katika shughuli za kijamii kama njia mojawapo ya kuwapatia wazai kipato.
Rai hiyo imetolewa na katibu Tawala mkoa Pwani,ndugu Zuberi Samataba wakati wa kilele cha maadhimisho wiki ya Elimu Mkoani Pwani .
Aidha alieleza kuwa wapo wazazi na walezi ambao wamekuwa chanzo cha kudidimiza Elimu ,kwa kuwaachia watoto kudhurura na kujihusisha na vigidoro na ngoma za usiku .“Serikali haiwezi kukubali mzazi akaachia mtoto kiholela ,watoto ni wa serikali ,mzazi yeyote atakayebainika kufanya hayo hatutamvumilia , kwani hii inasababisha kudumaza elimu katika mkoa wetu”Alisema Samataba.
Pia alizielekeza Halmashauri zote za Mkoa wa Pwani kuwachukulia hatua wazazi wote wanaowaachia watoto kushiriki katika shughuli za kijamii zisizo rasmi na hatarishi kwa maisha na ustawi wa watoto.Alikemea vitendo vya kupewa mimba za utotoni na maambukizi ya maradhi kwa watoto na amesisitiza kuchukuliwa hatua kali kwa wote wanaosababisha hayo .
Alisema kuwa, zipo taarifa kuwa wapo wazazi wanaojua watoto wao wanafanya vizuri darasani badala ya kuwasaidia wao huwakataza kufanya vizuri .
Naye kaimu Afisa elimu Mkoa wa Pwani ,bibi Hildegard Valerian Makundi alieleza kuwa uandikishaji wa wanafunzi wa elimu ya awali bado upo chini tofauti na wanaoandikishwa darasa la kwanza.
“ Lengo Serikali lilikuwa ni kuandikisha wanafunzi 35,418 kwa ajili ya Elimu ya awali ila walioandikishwa ni 26,997 sawa na asilimia 76 na uandikishaji darasa la kwanza lengo ilikuwa 47,686 walioandikishwa ni 52,551 sawa na asilimia 110” alieleza Hedegald.
Katika hatua nyingine Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoani Pwani ,Ramadhani Maneno alisema kuwa, ili kuhakikisha elimu inaboreshwa ni lazima kushirikiana wadau ,wazazi na walimu kutatua changamoto za kielimu badala ya kuiachia serikali pekee.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.