Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mheshimiwa Evarist Ndikilo amepokea vifaa Maalumu vya kunawia mikono kutoka Shirika la Nyumbu Kibaha (Tanzania Automotive Technology Center- TACT) ikiwa ni jitihada za Mkoa za kushirikisha wadau katika Mapambano dhidi ya maambukizi ya Virusi vya Corona.
Akizungumza wakati wa upokeaji wa vifaa hivyo kwa ajili ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Hospital ya Rufaa ya Tumbi.
Mhandisi Ndikilo amesema kuwa kifaa hicho kitaweza kusaidia sana watumishi na wageni mbalimbali wanokuja katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Hospitali ya Mkoa.
Pia ametumia wasaa huo kuendelea kuwakumbusha Wananchi wa Pwani kuwa waendelee kuchuka tahadhari ya kujikinga na ugonjwa huu.
“Napenda kuchua fursa hii kwa kuwakumbusha wananchi wote kuwa waendelee kuchukua tahadhari na kujiepusha na mikusanyiko na pindi mnapomuona mtu anadalili za ugonjwa huo msisite kutoa taarifa kwa mamlaka husika.
akishukuru shirika hilo Ndikilo alisema"endeleeni na Uvumbuzi huu kutengeneza vifaa hivi Mnao wahandisi wa kutosha si lazima tuagize kila kitu kutoka nje ya Nchi, asanteni sana tumevipikea vifaa hivi tutavitumia vizuri.
Akikabidhi msaada huo Meneja wa Masoko wa shirika la Nyumbu Bi Numwagile Mwaijumba alisema kuwa msaada huo wamekabidhi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Tumbi na Ofisi ya Mkuu wa mkoa kama njia mojawapo ya kuthibiti maambukizi ya Virusi vya Corona katika Mkoa wa Pwani.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.