Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mh. Mhandisi Evarist Ndikilo amezindua ugawaji wa Vitambulisho vya wafanyabiashara wadogo awamu ya pili. ambapo uzinduzi huo ulifanyika Mei 30 katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu wa mkoa.
Akikabidhi vitambulisho hivyo kwa Wakuu wa Wilaya Mhandisi Ndikilo amesema vitambulisho hivyo vimewasaidia wafanyabiashara kufanya biashara zao kwa urahisi na kuyafanya mazingira ya biashara kuwa rafiki kwani hakuna ushuru mwingine atakao tozwa mfanyabiashara baada ya kupata kitambulisho hicho.
Ndikilo amewahimiza wadau wote wanaohusika na zoezi hilo la ugawaji wa vitambulisho kutekeleza majukumu yao kikamilifu ili mkoa ufanye vizuri kitaifa.
Katika hatua nyingine Mhandisi Ndikilo ameeleza kuwa kwa mwaka 2019 Mkoa ulifanikiwa kugawa jumla ya vitambulisho 59,045 kati ya vitambulisho 60,000 sawa na asilimia 98 na kukusanya jumla ya shilingi bilion 1.1.
“ Nampongeza sana Mh. Rais wetu Mpendwa kwa maono makubwa aliyokuwanayo ya kuanzisha mfumo huu ambao umeonesha mafanikio makubwa na sisi kama wasaidizi wake katika Mikoa na Wilaya hatutamuangusha na tutaendela kutekeleza kikamifu maelekezo yake” alisema Ndikilo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.