Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo amesema kuwa Mkoa wa Pwani umedhamiria kuondoa kero ya Wanafunzi kukosa Madawati Mashuleni ifikapo Septemba Mosi 2020.
Akizungumza kwenye ziara yake Wilayani Bagamoyo Agosti 12 ,2020 wakati akikagua ukarabati wa shule ya Sekondari ya Bagamoyo, alieleza kuwa amekutana na Wahe. Wakuu Wilaya katika Kikao kazi Agosti 11, 2020 na kwamba wamekubaliana kuondoa changamoto ya madawati mashuleni ifikapo Septemba Mosi 2020.
Akitaja upungufu huo amesema Mkoa una upungufu wa madawati takribani 30,000 kwa shule za Msingi na 22,000 kwa shule za Sekondari.
Ndikilo amesema "Haiwezekani wanafunzi wakae chini wakati Mkoa tuna rasilimali za kutosha hususani Mazao ya Misitu na Viwanda. Tumekubaliana kama Mkoa kutumia Shirika la Nyumbu TACT (Tanzania Automotive Technology Centre Kibaha Mkoani kwetu kutengeneza Madawati hayo".
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.