Serikali Mkoani Pwani, imedhamiria kufungua Kisiwa cha Mafia katika nyanja ya Uchumi wa Bluu pamoja na kukitangaza ulimwenguni kupitia sekta ya utalii.
Akifungua tamasha la kisiwa cha Mafia la siku tatu linalolenga, kutangaza vivutio vilivyopo, mkuu wa mkoa wa Pwani Alhaj Abubakari Kunenge alieleza, Mafia ni kitovu cha uchumi wa bluu kati ya vivutio 82 vya utalii Mkoani humo.
"Rais Samia Suluhu Hassan anafanya kazi kubwa kulitangaza Taifa na kuvutia wawekezaji, mkoa kwa hili umejipambanua kuwa ukanda wa viwanda na sasa una viwanda 1,525 kati yake 240 ni vikubwa na vya kati":
"Juhudi zilizopo ni kuongeza nguvu sasa katika uwekezaji wa uchumi wa bluu,Mafia imetafsiriwa vizuri kwani adhma ya Rais ni kuona uwekezaji wa uchumi wa bluu nao unakua kwa kuongeza mahoteli ya kitalii, kuongeza idadi ya watalii, kutangaza uvuvi na samaki ikiwemo papapotwe anaepatikana kisiwani hapa"anasema Kunenge.
Awali Mkuu wa wilaya ya Mafia, Zephania Sumaye alieleza Mafia kijografia imependelewa kwa kuwa na kisiwa kikubwa na vidogo.
Zephania anawaomba , wawekezaji na watalii wa ndani na wa nje ya Mafia, kwenda Mafia kujionea vivutio mbalimbali .
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.