Vijiji 404 kati ya 417 Mkoani Pwani vimepata Umeme huku hali ya upatikanaji Maji ni ukiwa asilimia 86 mijini na 77 Vijijini.
Hayo yamebainishwa leo Oktoba 11, 2023 na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Abubakar Kunenge kwenye Mkutano Mkuu maalum wa kupokea Taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi - CCM ya 2020-2025 kwa Jimbo la Chalinze, Wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani.
Ameeleza kuwa kwa upande wa umeme kwa sasa vimebaki vijiji 13 tu ambavyo ni Visiwa na Delta na kuhusu maji vimebaki vijiji 29 ambavyo taratibu zao zinaendelea vizuri.
Naye Mhe. Dotto Biteko Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati amepongeza ameipongeza Halmshuri ya Wilaya ya Chalinze kwa Usimamizi wa fedha za Miradi na akawataka viongozi wote wa Halmashauri hiyo kushirikiana na kusema mazuri yaliyofanyika.
Naye Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dotto Biteko ameipongeza Halmshuri ya Wilaya ya Chalinze kwa Usimamizi wa fedha za Miradi na akawataka viongozi wote wa Halmashauri hiyo kushirikiana na kusema mazuri yaliyofanyika.
"Onesheni mliofanya kwa vitendo, msirudi nyuma bali sukumeni maendeleo ya wana-Chalinze mbele," amesema.
Katika hatua nyingine, Mhe. Biteko ameahidi kutoa Kompyuta 10 kwa shule ya Sekondari Moreto kwa ajili ya wanafunzi kujifunzia na akalielekeza shirika la umeme nchini - TANESCO kupeleka umeme katika shule hiyo.
Mhe Biteko pia amewataka watumishi wa Umma kutoka maofisini na kwenda kuwahudumia wananchi katika maeneno yao.
Amesisitiza jamii kuwa na upendo na kuheshimiana.
Mkutano huo pia umehudhuriwa na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.