Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani inaungana na Watanzania wote kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kutunukiwa Tuzo Maalumu ya Kimataifa ya The Global Goalkeeper Award.
Tuzo hii ni ishara ya kutambua mchango wake mkubwa katika maendeleo ya kijamii, hususan katika sekta ya afya, ambapo juhudi zake zimefanikisha kupungua kwa vifo vya mama wajawazito na watoto wachanga chini ya umri wa miaka mitano.
Tuzo hiyo, ambayo hutolewa kwa viongozi waliowezesha nchi zao kuharakisha maendeleo kuelekea kufanikisha Malengo ya Maendeleo Endelevu (Sustainable Development Goals – SDGs), imekabidhiwa kwa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na Dkt. Anita Zaidi, Rais wa Kitengo cha Usawa wa Jinsia kutoka Taasisi ya Bill & Melinda Gates Foundation.
Akizungumza kuhusu tuzo hiyo, Mheshimiwa Rais Dkt. Samia amesema kuwa kati ya mwaka 2020 hadi 2024, uwekezaji uliofanywa na Serikali katika sekta ya afya umewezesha Tanzania kuongeza idadi ya vituo vya kutolea huduma za dharura kwa mama na mtoto kutoka 340 hadi 523.
Tunampongeza kwa dhati Mheshimiwa Rais kwa heshima hii kubwa, ambayo inaendelea kuiweka Tanzania katika ramani ya dunia kwa juhudi zake za kuleta maendeleo na ustawi kwa wananchi wake.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.