Mkuu wa Mkoa wa Pwani ,Mhandisi Evarist Ndikilo,ametoa onyo kwa mtu atakaejaribu kuzuia watoto ,kupata chanjo ya kuzuia saratani ya mlango wa kizazi, ambapo zoezi hilo linatarajiwa kuzinduliwa kimkoa april 30 mwaka huu .
Aidha ameeleza saratani hiyo ndiyo inayoongoza kwa kuua wanawake wengi ukilinganisha na saratani nyingine Tanzania,hivyo kuna umuhimu wa kuzuia ugonjwa huo kwa watoto hao.
Akifungua mkutano wa wadau wa chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi Mkoani Pwani, Mhandisi Ndikilo alisema kuwa , wazazi na walezi wahakikishe watoto wa kike waliofikisha miaka 14 wanaenda katika vituo vya kutolea huduma za chanjo ikiwemo vituo vya afya kwa ajili ya kupaiwa chanjo hiyo.
“Kamwe asiwepo mtu wa kuzuia watoto wetu ambao ni Taifa la Leo na Kesho kupata kinga hii muhimu ili kuepuka madhara makubwa yanayoweza kuwapata hapo baadae”alisisitiza Ndikilo.
Hata hivyo aliwahakikishia wananchi kuwa chanjo hiyo ni salama na haina madhara yoyote kwa walengwa ,kwani hutolewa na wataalamu wenye uzoefu mkubwa waliobobea katika fani hiyo .
Mhandisi Ndikilo aliwataka wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa halmashauri kusimamia utekelezaji wa zoezi hilo ili serikali ipate matokeo chanya na makubwa katika kukabiliana na tatizo hilo.
Alisema kuwa,Serikali imeamua kuanza kutoa chanjo hiyo,”: na nichukue fursa hii kuipongeza wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii ,Jinsia ,Wazee na Watoto kwa kushirikiana na wadau mbalimbali katika jitihada za kuboresha afya ya mabinti nchini ikiwa ni pamoja na kupunguza vifo vitokanavyo na saratani kwa kuanzisha chanjo dhidi ya saratani hiyo".
Aidha aliwaomba viongozi wa dini na viongozi mbalimbali kusaidia kupeleka ujumbe kupitia mihadhara na mikutano juu ya uanzishwaji wa chanjo hiyo.
Nae mratibu wa afya ya uzazi na mtoto mkoani humo ,Bi.Joyce Gordon alisema akinamama wengi ambao wapo kwenye hatari ya kuugua kansa ni wale wenye virusi vya ugonwja wa UKIMWI.
Pamoja na hilo,alisema wagojwa walioingiakatika Hospitali ya Ocean road tangu mwaka 2006 -2016 ,inaonekana kansa inayoongoza ni ya mlango wa kizazi.
Bi.Joyce alielezea kuwa, takwimu za mwaka 2006 saratani hiyo ilikuwa ikiongoza ikifuatiwa na saratani ya matiti.
Alisema makisio ya ukubwa wa tatizo kwa mwaka 2002 yalikuwa ni zaidi ya 7,000 ambapo ikifikia 2025 makisio yanatarajia kufikia 12,416 hivyo inaonyesha tatizo kuzidi kukua.
Kwa upande wake mratibu wa chanjo mkoani Pwani,Abbas Hincha aliweka bayana kuwa walengwa wa chanjo hiyo kwa mwaka huu ni wasichana wote wenye miaka 14.
Hincha alisema wanatarajia kutoa chanjo kwa wasichana wasiopungua 18,823 katika mkoa huo
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.