Mkoa wa Pwani, umepata mauzo kilo milioni 6.5 sawa na sh.bilioni 18 katika minada miwili ya awali kwa msimu wa mwaka huu 2022/2023.
Hayo yamebainika wakati mkuu wa Mkoa wa pwani abubakar kunenge akikabidhi pikpiki tisa kwa maafisa ushirika wa halmashau za mkoa huo .
Kunenge alisema ,hili Ni ongezeko na neema kwa wakulima wa Ufuta tofauti na msimu uliopita wa mwaka 2021 ambapo Tani 13,000 ziliuzwa na kupatikana zaidi ya sh.Bilioni 28.
Mkuu huyo wa Mkoa alieleza , maafisa wa Ushirika ,maafisa ugani watapimwa kwa usimamizi wao kwa kuangalia hali ilivyo Sasa ,matarajio na baada ya kupatiwa vifaa hivyo ili kuleta matokeo chanya.
Awali Mrajisi Msaidizi Mkoani Pwani, Angela Nalimi alitaja changamoto za usimamizi wa shughuli za ushirika kutokana na uhaba wa vitendea kazi ikiwemo usafiri na kumshukuru Rais kwa kutoa usafiri kupitia Wizara ya Kilimo pamoja na Tume ya Maendeleo ya Ushirika.
Akipoke Pikipiki hiyo Ofisa ushirika wa Halamshauri ya Chalinze Raphael Kajale amesema kuwa usafiri huu umekuja wakati muafaka kwani , katika Halmashauri yake kuna kata kumi na tano ambazo nyingi zipo pembezoni hivyo pikipiki hizi zitasaidia kutekeleza katika majukumu yao ya kikazi kwa wakati.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.