Mkoa wa Pwani ni miongoni mwa Mikoa nchini, yenye idadi kubwa ya wagonjwa wenye vikope(Trachoma) huku wilaya inayoongoza ikiwa ni Mkuranga yenye wagonjwa hao 1,041,wilaya ya Rufiji 191,Kisarawe 243 na Kibiti 207.
Hayo yalibainika katika kampeni ya kutokomeza ugonjwa wa vikope iliyozinduliwa wilayani Mkuranga mkoa wa Pwani.
Mkuu wa Mkoa Pwani, Mhe. Mhandisi Evarist Ndikilo akiwa ni mgeni rasmi katika uzinduzi huo aliitaka jamii kuachana na imani potofu na badala yake wajitokeze kupima ugonjwa huo ili kuweza kupatiwa matibabu na kuondokana na upofu .
Aidha, alitoa rai kwa viongozi wa kijamii kuwapeleka wagonjwa wenye vikope katika kambi za uchunguzi ili kupatiwa matibabu.
Nae meneja mradi wa IMA WORLD HEALTH, Alex Msumanje akielezea magonjwa yasiyopewa kipaombele aliyataja kuwa ni matende,mabusha,minyoo ya tumbo,kichocho,usubi na trachoma(vikope).
Kaimu mratibu wa magonjwa yasiyopewa kipaumbele wizara ya afya Oscar Kaitaba alisema watu takribani 11,350 wameshafanyiwa urekebishaji wa kope katika wilaya 21.
Aidha aliwaomba wananchi kujitokeza kufanyiwa urekebishaji wa kope zao kwani huduma hiyo ni bure na mradi huu unafanywa katika mikoa 6 ikiwemo Manyara,Lindi ,Pwani Arusha,Mtwara,na Dodoma.
Kampeni hiyo katika Mkoa wa Pwani itafanyika kwenye Wilaya nne ikiwa ni pamoja na Kibiti,Kisarawe,Mkuranga na Rufiji na itahusisha magonjwa yasiyopewa Kipaumbele kama Matende na Mabusha,Minyoo ya Tumbo, Usubi,Kichocho na Vikope (Trachoma)
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.