RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameendelea kufungua milango kwa wahisani na wadau wa maendeleo kupitia Sekta binafsi ili kumuunga mkono jitihada za Serikali kutoa huduma kwa watanzania.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava,alieleza hayo wakati Mei 2, 2024 alipokuwa halmashauri ya Mji Kibaha, kuzindua mradi wa kisima kirefu cha maji shule ya msingi Visiga, mradi ambao umegharimu 16.870 kutoka kwa mfadhili Taasisi ya REHEMA FRIENDSHIP AND SOLIDARITY TRUST.
Mzava alitoa wito wahisani na wafadhili mbalimbali kuendelea kukaribishwa maana milango ipo wazi kwani Serikali yetu imeshafungua mlango .
Vilevile, alieleza Serikali, wahisani, wadau wanapotoa fedha za miradi wanapenda kuona inalindwa na kutunzwa ili idumu kwa kipindi kirefu.
Awali akitoa taarifa ya mradi huo, Mwalimu Mkuu Shule ya msingi Visiga, Mwalimu Ali Seif Ali alieleza, kisima kinafaida kubwa ni mkombozi mkubwa kwa wanafunzi na walimu pamoja na jamii inayozunguka shule kwa kupunguza changamoto ya maji.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.