Katibu Tawala Mkoa wa Pwani Dkt Delphine Magere amewaomba wadau mbalimbali kujitokeza kusaidia mapambano dhidi ya ugonjwa wa Covid-19 hasa katika kituo cha matibabu Wagonjwa wa virusi Corona cha Lulanzi kilichopo Wilayani Kibaha.
Aliyasema hayo mjini Kibaha wakati akipokea vifaa mbalimbali kutoka timu ya kampeni ya Mikono Safi Tanzania Salama ambapo msanii Mrisho Mpoto alikabidhi vifaa hivyo ikiwemo vitakasa mikono lita 150 pamaoja na Dispensa 5 kwa ajili ya kutolea vitakasa mikono.
Dkt Magere alisema kuwa vita hiyo ni watu wote katika kupambana na ugonjwa huo kwani misaada kama hiyo inahitajika kwa wananchi wa mkoa huo pamoja na wagonjwa kwenye kituo hicho.
“Mahitaji ni makubwa kuanzia Barakoa, Vitakasa mikono, Sabuni na maji kwa kituo chetu cha kuhudumia Wagonjwa wa Covid -19 hivyo wadau mbalimbali wanapaswa wajitokeze,’’alisema Dkt Magere.
Aidha alisema kuwa wanaishukuru kampeni hiyo kwa kuusaidia Mkoa huu vifaa hivyo ambavyo vitasaidia mapambano hayo dhidi ya Ugonjwa huo ambao umesbabisha watu wengi kuishi kwa hofu.
“Pamoja na vifaa hivi tunapaswa kuchukua tahadhari ikiwa ni pamoja na kuvaa barakoa kuepuka misongamano, kutumia vitakasa mikono na kunawa kwa maji yanayotiririka na sabuni,” alisema Dkt Magere.
Naye Anyitike Mwakitalima ambaye ni mkuu wa kitengo cha Maji na usafi wa mazingira Wizara ya Afya maendeleo ya jamii Jinsia Wazee na Watoto alisema kuwa timu hiyo inahamsisha na jamii juu ya tahadhari dhidi ya Corona.
Mwakitalima alisema kuwa wmaefanya kampeni kwenye mikoa ya Mbeya, Songwe, Dar es Salaam na Pwani kwa ajili ya elimu ya tahadhari juu ya Ugonjwa huo pia kutoa vifaa vikiwemo vya kutumia vitakasa mikono.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.