Katibu Tawala Mkoa wa Pwani Pili Mnyema amesisitiza umuhimu wa watumishi kuwajibika kwa kufanya kazi kwa uadilifu, kuzingatia kanuni, taratibu, sheria na miongozo ya utumishi wa Umma.
Mnyema ametoa msisitizo huo leo Agosti 26, 2025 wakati akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Mji wa Rufiji ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kuzitembelea Halmashauri zote za Mkoa huo inayohusisha pia ukaguzi wa miradi ya maendeleo.
"Uadilifu ni pamoja na kuwa mnyenyekevu, kuepuka rushwa, ubadhirifu na kutosababisha maumivu kwa watumishi mwenzako," alisema.
Pia amesisitiza watumishi kuzingatia ushirikiano, upendo, kanuni za mavazi yenye staha na mawasiliano rafiki.
Msisitizo mwingine ni juu ya uzingatiaji matumizi ya mifumo ya Serikali kama ule wa manunuzi akisema "manunuzi yasifanyike nje ya mfumo, taratibu za manunuzi zifanyike kwa wakati ili miradi itekelezwe na kukamilika kwa wakati."
Katika ziara hiyo, Mnyema alitembelea na kukagua miradi ambayo ni Hospitali ya Wilaya ya Rufiji, Shule ya Sekondari ya Wasichana Bibi Titi Mohamed, Mradi wa maji Nyanda Katundu, ranch ndogo za Kijiji cha Nyamwage, barabara ya Mahakamani, Hospitali na Kaunda pamoja na Jengo la Utawala Halmashauri ya Mji Rufiji.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.