Katibu Tawala Mkoa wa Pwani Pili Mnyema amewaelekeza wataalamu wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti kuwa wabunifu kuibua Miradi mbalimbali ya Maendeleo kulingana na fursa zilizopo kwenye kwenye eneo lao ili kuongeza mapato ya Halamashauri hiyo.
Mnyema ametoa maelekezo hayo leo Agosti 27, 2025 wakati akizungumza na wakuu wa Sehemu na Vitengo katika ofisi ya Mkurungezi wa Halmashauri ya hiyo.
“Tunakazi ya kufikiria kutoka kutegemea Serikali Kuu pekee kuleta fedha za utekelezaji wa Miradi badala yake tubuni miradi mipya itakayoweza kuongeza mapato, mfano ni kuandaa zaidi maeneo ya uwekezaji ili tuweze kutekeleza miradi ya maendeleo itakayoweza kusaidia wananchi wetu,” Alisema Mnyema.
Aidha amesistitiza kuendeleza pia fusra za asili zilizopo kwa kutumia mbinu za kisasa zitakazowezesha kilimo kuendelea kuzipatia halmashauri hizo mapato hata kama kutatokea mabadiliko ya tabia nchi.
Akizungumzi Ukusanyaji wa Mapato Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Hanan Bafagih amesema kwa mwaka wa fedha 2024/25 Halmashauri hiyo ilikusanya kiasi cha shilingi billioni 2.9 ambapo makisio yalikuwa kukusanya bilioni 2.8 nakwa mwakuu huu wa fedha halmashauri hiyo inatarajia kukusanya zaidi ya Bilioni 3.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.