KatibuTawala mkoa wa Pwani,Zuwena Omary ameyataka Mashirika yasiyo ya kiserikali kuboresha mawasiliano na Serikali katika kutoa taarifa sahihi za utekelezaji wa shughuli wanazozifanya .
Hayo ameyasema Leo Septemba 19,2022 katika Mkutano Mkuu wa Mwaka wa kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Mashirika yasiyo ya kiserikali kwa kipindi cha Januari hadi Desemba 2021,ulioandaliwa na ofisi ya Mkuu wa mkoa huo, ambapo wawakilishi wa Mashirika 45 walihudhuria .
Alielezea kwamba ,wahakikishe Serikali inapata taarifa za uwazi na ukweli pamoja na changamoto zinazowakabili ili ziweze kutatuliwa.
Zuwena alisema, kwa kutokuwa wawazi na wakweli inasababisha mkoa kutokuwa na taarifa sahihi kwani kwa taarifa zilizopo Kuna Mashirika yalisajiliwa kufanya kazi Mkoani Pwani 300 wakati yanayofanyakazi 82 pekee.
"Mashirika mengine hayafanyi kazi zaidi ya hayo 82, yalianza Lakini yamekwama,Lazima tujitafakuri kwanini hatufikii malengo"
"Kuna Mashirika yasiyo ya kiserikali ambayo yanakihusisha na masuala ya madawa ya kulevya, watoto, wanawake,vijana ,ustawi wa jamii na afya Lakini ukiuliza taarifa zao unakuta hawafanyi shughuli lengwa walizojisajili kuzifanya ndani ya jamii zao"alisema Zuwena.
Akitoa taarifa ya usajili wa Mashirika hayo katika mkoa huo, Msajili Msaidizi wa Mashirika yasiyo ya kiserikali Mkoani hapo, Mgeni Kisanga alisema kuwa , hadi sasa takwimu zinaonyesha Kuna Mashirika 300 kati ya hayo 82 ndio yapo hai.
Mgeni alifafanua kwamba , miradi iliyotekelezwa ni 104 yenye thamani ya sh.bilioni 1.6.
Mashirika yasiyo ya kiserikali Mkoani humo, yameeleza wanakabiliwa na changamoto ikiwemo Ukosefu wa elimu katika Uelewa wa miongozo na sheria sahihi na kanuni juu ya sekta hiyo hali inayosababisha kufungiwa na wengine Kuwa na madeni makubwa ya Mamlaka ya mapato , pamoja na kushindwa kujiendeleza baada ya wafadhili kusitisha ufadhili.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.