Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge ameueleza uongozi wa Kampuni ya Lake Agro Investment Ldt inayoanzisha kilimo cha miwa na kujenga kiwanda cha Sukari Wilayani Rufiji kuwa Matarajio ya Mkoa na Serikali ni kuwapatia wanachi, utaalam, Kodi na mchango wa maendeleo kwenye miradi ya jamii.
Kunenge aliyasema hayo Juni 17 alipotembelea eneo la mradi huo uliopo kwenye Vijiji vya Nyanda na Utunge Kata ya Chemchem Wilayani Rufiji na kujionea matayarisho ya awali yanayofanywa na kampuni hiyo inayotarajia kulima miwa, kuzalisha na kuchangia kuondoa nakisi ya Sukari nchini na kuuza ziada nje ya nchi.
“Zaidi ya watu 18,000 wanatarajiwa kupata ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja, Wananchi wetu watapata utaalamu kutokana na teknolojia ya kisasa itakayotumika, kutakuwa na wakulima wengine wa nje Outgrowers ambapo mwekezaji yupo tayari kuwapa msaada wa kitaalamu ili wachangie kuuza miwa kiwandani, pia kutakuwa na Mchango (CSR) wa wawekezaji hawa kwa Jamii." alifafanua RC Kunenge.
Ili kuwezesha mazingira ya uwekezaji na ya jamii kuwa mazuri, Kunenge amesema kuwa wamekubaliana na Uongozi wa Wilaya ya Rufiji kupima eneo lote linalozunguka Mradi huo.
"Tumekubaliana kwa sababu mradi huu ni Mkubwa paanze kupimwa na kupangwa tupate mji unaojitegemea,tupate Maduka sehemu za huduma za Jamii Masoko na makazi ya watu." Alifafanua kunenge
Awali, akitoa taarifa ya uwekezaji, Meneja wa Mradi huo Bw. Abubakar Nassor Manager alibainisha kuwa wanatarajia kulima miwa kwenye enoeo la hekta 15,000 na kiwanda kitazakuwa na uwezo wa kuzalisha sukari tani laki 1 kwa mwaka.
Nassoro amemshukuru Mhe Rais Samia Suluhu Hassan kwa Mazingira mazuri ya Uwekezaji na Ushirikiano wanaoupata kutoka Uongozi wa Mkoa. Wa Pwani na akatoa wito kwa Wananchi kuchangamkia fursa hiyo ya kiuchumi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.