Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge, ameagiza kuchukuliwa hatua wale wote wanaobainika kusababisha hasara kwenye hoja za ukaguzi wa mahesabu na kuhakikisha hoja zote ambazo hazijafungwa zifungwe ifikapo September 30 mwaka huu.
Vilevile ameagiza Halmashauri zote Mkoani hapo ,kuweka vipaumbele ,kupanua wigo wa vyanzo vipya vya mapato na Kuwa wabunifu ili kukuza uchumi na kuongeza uwezo wa Halmashauri .
Akizungumza na madiwani na watendaji wa Halmashauri ya wilaya Mkuranga wakati wa Kikao Maalumu cha Kujadili Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Juni 20, 2022 Kunenge aliwaasa watendaji kujenga tabia ya kuhifadhi na kutunza nyaraka ili kuepusha hoja ambazo zipo ndani ya uwezo wa kuzifunga.
Alionya kuacha kufanya kazi kwa mazoea na kupuuzia mambo kwani kwa kufanya hivyo kunasababisha Ujibuji wa Hoja za ukaguzi kukwama.
Kuhusu mabadiliko ya kiuchumi mkoa , Mkuu huyo wa mkoa alisema ni wakati wa kufanya mabadiliko ya kasi za ufanyaji kazi ili kupiga hatua zaidi ya kimaendeleo na kiuchumi.
"Watendaji na wataalamu muwe wabunifu unaoendana na spidi ya Serikali na Rais Samia Suluhu kuleta matokeo chanya kwa wananchi," Mkoa bado unahitaji nguvu ya pamoja kuinua uchumi,'"! ambao bado kimkoa haupo vizuri kwani Hadi Sasa Mkoa unachangia 1.94% kwenye GDP alifafanua Kunenge.
Pia aliwasisitiza kuweka mikakati ya kutekeleza mpango wa kuboresha Mazingira ya Biashara (Blue Print) ili kukuza mapato.
Ameisisitiza Halmashauri hiyo kuwa na Vipaumbele vyenye tija kwa Kuzinga Blue Print na vipaumbele vya Mhe. Rais ili kupata matokea makubwa na kwenda sambamba na maono ya Mhe. Rais.
Sambamba na hilo RC Kunenge aliitaka Halmashauri hiyo kuweka Mazingira Bora ya kuvutia wawekezaji pamoja na kutangaza fursa mkoa.
Mkaguzi Mkuu wa nje Mkoani Pwani ,Mary Dibogo ameipongeza Halmashauri hiyo kwa kupata hati safi kwa mara ya sita mfulululizo.
Alitoa Rai kwa Halmashauri hiyo kuwa bado Kuna hoja hazijafungwa ,wafunge hoja zilizobaki kwa muda waliopewa .
Awali Akiwasilisha taarifa Mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za Halmashauri ya wilaya Mkuranga kwa mwaka wa 2020/2021 Mkaguzi mkuu wa Ndani Faidha alisema kuwa Halmashauri ya Mkuranga ilikuwa na Hoja 64 kati ya hizo 32 zimejibiwa na 32 bado hazijapatiwa majibu
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.