Mkuu wa Mkoa wa Pwani mhe Abubakar Kunenge, 2022 amekutana na kufanya Mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania (CTI) Leodgar Tenga.
Akizungumza kwenye kikao hicho Juni 15 Kunenge, ameeleza kuwa Amefanya Jitihada za kukutana Uongozi huo kwa sababu Mkoa wa Pwani ni Mkoa Uwekezaji hususan Viwanda ambapo hadi sasa wanaviwanda 1453 ambapo Viwanda vikubwa ni 87.
Ameeleza kuwa Mkoa wa Pwani kwa kushirikiana na TIRDO tayari wameandaa Ramani ya Uwekezaji wa Viwanda (Industrial Mapping) inayoonesha Viwanda vilipo, Upatikanaji wa Malighafi na kurahisisha kufika Viwandani hapo. Amemwomba waangalie namna ya kushirikiana na Mkoa kuzindua Mpango huo.
Ameeleza kuwa katika ziara yake Viwandani Changamoto kubwa alizokutana nazo ni Changamoto ya Umeme, Maji, na Barabara.
"Wawekezaji wamesema tukiwapa umeme wataongeza Uwekezaji"
Ameeleza kuwa Wawekezaji wanalalamikia Muda mwingi kutumia kupasha moto mitambo yao na pindi wakianza uzalishaji Umeme unakatika.
Ameeleza kuwa Serikali imeipa Kipaumbele Mkoa wa Pwani katika Upatikanaji wa Umeme, Maji na Barabara.
Aidha Mkuu huyo wa Mkoa ameeleza Mikakati ya Mkoa wa Pwani ni Kuvutia na Kuongeza Uzalishaji kwa Viwanda Vilivyopo.
“Lazima tuwe na Mikakati ya kuvutia na kutaka viongezeke(Growth) kama mwekezaji amepanga kupata faida ndani ya miaka mitatu tutawasaidia, Sisi iwe sababu ya wao kuongezeka" Ameeleza Kunenge.
Amemweleza azma yake ya kuboresha Vikao vya Mabaraza ya Biashara ya Mkoa Ili viwe na Tija."Tatizo la Vikao hivi tukiitisha wanahudhuria watumish wa chini Wawekezaji, tunaangalia Upya Ameeleza Kunenge.
Aliendelea kusema kuwa, Mkoa huo upo kwenye Mpango wa kupanga Mji mpya wa kibiashara (Kwala Commercial City) uliopo Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha ambapo kutakuwa na Uwekezaji Mkubwa wa Viwanda vikubwa 350, Bandari kavu ya Kwala na kituo cha kuunganisha Vichwa vya Treni (marshalling Yard) Barabara ya Zege kutoka Vigwaza hadi Eneo la Industrial Park,na Nchi Jirani kuwa na maeneo kwenye eneo hilo kuhifadh Mizigo yao.
Amemweleza kuwa Mkoa huo unatatajia kuwa na Wiki ya Maonesho makubwa ya Viwanda Biashara na Uwekezaji Mkoa wa kuanzia Tarehe 1 -6 Sept 2022 katika Viwanja vya Sabasaba Mkuza Kibaha.
"Nawaeleza haya yote CTI ili mpate kushiriki katika Fursa hizi zote na Sehemu yenu ya kuonesha kazi zenu iwe Mkoa wa Pwani.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa CTI Bw. Leodgar Tenga amemshukuru Mhe Mkuu wa Mkoa kwa mapokezi, Ameeleza kuwa amekuja ili awe karibu na Uongozi wa Mkoa wa Pwani katika kutatua Changamoto za Wawekezaji wa Viwanda Mkoani Pwani. Ameeleza kuwa CTI Sasa itakuwa na wajibu wa kutangaza hayo yote na kushirikiana kikamilifu na Mkoa huo ikiwemo kuandaa Maonesho ya Viwanda na kupanga Mji mpya wa kibiashara wa Kwala.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.