Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhe. Abubakar Kunenge, amefungua mafunzoya siku moja kuhusu Elimu ya Uraia, Utawala Bora, na Haki za Binadamu kwaviongozi wa Halmashauri za Mkoa wa Pwani. Mafunzo hayo yalifanyika katikaukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Kibaha, yakiratibiwa naWizara ya Katiba na Sheria.
Katika hotuba yake ya ufunguzi, Mhe. Kunenge alisisitiza umuhimuwa viongozi kufuata misingi ya haki, sheria, na kanuni za utawala bora ilikuleta mabadiliko chanya katika jamii wanayoiongoza. Aliwataka viongozi haokutekeleza majukumu yao kwa uwajibikaji na kuzingatia mahitaji ya wananchikabla ya kufanya maamuzi.
Serikali imejizatitikutoa mafunzo haya ili kuwajengea viongozi uelewa wa kina kuhusu misingi yahaki na utawala bora. Ni lazima tusikilize wananchi na kuzingatia maoni yaokatika uamuzi wowote. Wajibu wenu ni kujifunza na kuleta matokeo chanya;tujipime kwa kuona ni wananchi wangapi wameridhika na utendaji wetu,†alisemaMhe. Kunenge.
Aidha, alisisitiza kuwa viongozi wanapaswa kufanya kazi kwakuzingatia vipaumbele vya wananchi na kufuata maadili ya utendaji, hukuwakitafuta suluhisho la changamoto zinazowakabili.
Lazima tujue vipaumbelevyetu na kuwa na uthubutu wa kufanya kazi yenye tija. Kiongozi mzuri ni yuleanayebadilisha maisha ya wananchi kwa vitendo, si kwa maneno pekee,â€aliongeza.
Mafunzo haya yaliwahusisha Kamati ya Usalama ya Mkoa, viongoziwa wilaya, na watendaji wa kata kutoka Halmashauri mbalimbali za Mkoa wa Pwani,pamoja na wataalamu wa sheria na utawala bora.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Katiba naUfuatiliaji wa Haki, Bw. Lawrence Kabigi, alieleza kuwa lengo kuu la mafunzohaya ni kuwajengea viongozi uelewa wa kina kuhusu misingi ya demokrasia,utawala bora, na haki za binadamu ili kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.
Ni muhimu kwa viongozi kukumbushana mara kwa mara majukumu yaoili kuongeza umakini na ufanisi katika utendaji wa kazi. Tunatarajia kuwa baadaya mafunzo haya, viongozi watazingatia haki za binadamu, utawala wa sheria,ushirikishwaji wa wananchi katika maamuzi, na uwajibikaji wa viongozi kwajamii,†alisema Bw. Kabigi.
Aidha, aliwashukuru viongozi wa Mkoa wa Pwani kwa ushirikianowao katika kufanikisha mafunzo hayo na kusisitiza kuwa Serikali itaendeleakutoa mafunzo kama haya ili kuhakikisha misingi ya utawala bora inazingatiwakatika kila ngazi ya uongozi.
Mafunzo hayo yaliangazia mada mbalimbali, zikiwemo utawala washeria, uwajibikaji wa viongozi, ushirikishwaji wa wananchi katika maamuzi, naumuhimu wa kuheshimu haki za binadamu katika utendaji wa Serikali.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.