Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Abubakar Kunenge amewasilisha taarifa ya mapokezi ya Wanafunzi wa Kidato cha kwanza na darasa kwanza 2024 pamoja na utekelezaji wa Miradi ya Ujenzi wa miundombinu ya Elimu.
Mhe Kunenge amewasilisha hayo kwenye kikao kwa njia ya Mtandao na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI ambapo amesema Mkoa wa wa Pwani unamalengo ya kuandikisha wanafunzi wa awali 55771 hadi kufikia tarehe 29 mwezi huu jumla ya wananfunzi 25136 wameandikishwa ikiwa ni asilimia 45.1 na uandikishaji unaendelea.
Aidha amesema Mkoa una malengo wa kuandikisha wanafunzi wa Darasa la kwanza 51446 na hadi sasa wanafunzi 37694 wamekwisha andikishwa sawa na asilimia 73.3 na uandikishaji unaendelea mpaka tarehe 31 mwez machi mwaka ujao.
RC kunenge ameeleza pia wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha akwanza mwaka 2024 kwa shule za kutwa na shule teule ya Mkoa ni 40,796 na ufaula kwa sasa ni asilimia 83.7.
Katika hatua nyingine RC kunenge amemuhakikishia Mhe. Waziri kuwa wanafunzi wote waliochaguliwa kuniunga na kidato cha kwanza wataendelelea na masomo yao bila ya kikwazo chochote.
Pia kwa upande wa miundombinu Kunenge ameeleza kuwa mkoa umepokea jumla ya Bilion 29.7 ambapo ameeleza fedha hiyo ni kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu mbalimbali ya Elimu ikiwa ni Ujenzi wa shule mpya 36. Vyumba vya madarasa 198, Nyumba za walimu 13 mtundu ya vyoo 269 ,Mabweni 21 vituo vya Walimu TRC 13.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.