Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge ameiagiza Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe kuhakikisha kinasimamia Marejesho ya fedha shilingi Milioni 473 ambazo ni makusanyo ya fedha za ndani zilizokusanywa na kutokupelekwa Benki hali iliyopelekea Halmashauri hiyo kupata hati ya Ukaguzi yenye mashaka.
Pia ameiagiza kuchukuliwa kwa hatua kali za kisheria kwa wahusika wote walioshiriki kuchukua fedha hizo na kusababisha Hasara Halmashauri hiyo.
RC Kunenge alitoa agizo hilo Juni 20, 2022 wakati alipohutubia kikao maalum cha Baraza la madiwani kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe kilichokaa kupitia na kujadili Taarifa za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali za Mwaka 2020/2021 ambapo Halmashauri hiyo imapata hati yenye Mashaka.
"Ni kwanini Wameacha mpaka haya yakatokea, Wataalam hamkufanya Wajibu wenu"Ameeleza Kunenge.
"Mkaguzi wa Ndani wa Halmshauri aliwashauri lakini hamkuchukua hatua, Mkaguzi wa Ndani alifanya kazi nzuri" nampongeza alisema Kunenge
"Maagizo yangu Fedha Shilingi Milion 473 hizo zirudi ifakapo Septemba 2022 na hatua za kisheria zichukuliwe kwa wote waliosababisha haya "Ameeleza Kunenge.
Nae kwa upande wake Mkaguzi Mkuu wa nje Mkoani Pwani ,Mary Dibogo aliitaka halmashauri hiyo kutoa ushirikiano mzuri pindi wanapokuja kufanya ukaguzi kwani hii itasaidia kuondoa kasoro ndogo ndogo zinazopelekea kupata hati yenye mashaka
Awali ikiwasilishwa haarifa hiyo ya mdhibiti na mkaguzi wa hesabu za Serikali CAG ya mwaka wa fedha 2020/2021 ilieleza kuwa Halmashauri ya kisarawe ilikuwa na Hoja 39 kati ya hizo 15 zimefutwa na 24 hazijapata majibu na kati hizo hoja 6 tu ndio zipo ndani ya uwezo wao.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.