Serikali Mkoani Pwani, imeonya watu wasio wazalendo ambao wamekuwa wakisambaza kwenye mitandao ya kijamii taarifa za uongo kuhusiana na kutekwa kwa watoto kitendo ambacho kinasababisha taharuki kwa wazazi na jamii.
Vilevile imekemea, watu wanaojihusisha na utekaji watoto, kuacha tabia hiyo kwani atakaebainika atakamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria.
Mkuu wa mkoa wa Pwani, alhaj Abubakar Kunenge ametoa onyo hilo Kibaha Mkoani Pwani kwenye maadhimisho ya siku ya mashujaa.
Ameeleza vyombo vya dola, Jeshi la polisi mkoa wa Pwani vimejipanga kudhibiti na vina vina weledi mkubwa, Teknolojia ya kutosha kubaini watu wanaojirekodi na kusambaza uongo.
Kunenge alifafanua kuwa, wanajua kila kinachoendelea hivyo wanaomba ushirikiano kwa wananchi kuzuia na kutoa taarifa za vitendo vya aina hiyo kwenye maeneo yao.
Aliomba endapo jamii ikibaini wauaji wa wenye ulemavu wa ngozi, utekaji watoto, mauaji, vitendo vya unyanyasaji watoto na wanawake wafichue vitendo hivyo ili watuhumiwa wakamatwe na wachukuliwe hatua za kisheria.
"Kuna sura mbili katika ya masuala ya utekaji, kuna ukweli yapo matukio ya utekaji ambayo tunakemea kwa nguvu zote kwa wanaojihusisha"
"Lakini kuna sura nyingine kwa baadhi ya watu wanaokwenda na upepo wa matukio hayo ambao wanaojirekodi kusema uongo kuwa kuna watoto wametekwa, Tuzuie vitendo hivi,tushirikiane kutoa taarifa kwa watu wanaoleta taharuki ,lakini tukiwabaini tusijichukulie sheria mkononi ""alisisitiza Kunenge.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.