Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Abubakar Kunenge amekutana na wadau, wafanyabiashara na wawekezaji kwenye kikao cha pili cha Uwekezaji, Biashara na Shirika la Viwanda Vidogo( SIDO) Kanda ya kusini-Mashariki katika kikao maalum kilichofanyika leo septemba 15 ,2022 katika ukumbi wa mikutano uliopo katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Pwani.
Katika kikao hicho kunenge ametoa taarifa kamili kuhusu tarehe rasmi ya wiki ya Uwekezaji na Biashara kuwa ni tarehe 5 hadi 10 Oktoba, 2022 .
Kunenge ametumia nafasi hiyo kuwaeleza wadau wote kuwa lengo kubwa la maonesho ya Uwekezaji na Biashara ni kutafuta masoko, fursa ya kupata malighafi kwaajili ya viwanda na kutafuta wawekezaji .
Kunenge , amewaeleza wadau kuwa Pwani ni Mkoa unaongoza kwa viwanda ikiwa na jumla ya viwanda 1490 kati ya hivyo viwanda 90 ni viwanda vikubwa pia maonesho hayo yatadhibitisha ni kiasi gani sera ya viwanda inavyofanya kazi vizuri " maonesho hayo hayawezi kufanyika bila wawekezaji kuja."
Amesema, kama timu ikiindwa vizuri basi kiongozi wa Kitaifa akija dunia nzima itaifahamu Pwani kwani dunia ni Kijiji .
Aidha, Kunenge amesema,tarehe 8 /10/2022 kutakua na kongamano litasimamiwa na wataalam waliobobea katika masuala ya uchumi taaluma mbalimbali zitaoneshwa
Pia amesisitiza kwa upande wa ulinzi na usalama upo vizuri.
Mhe. Kunenge awashukuru wadau, wawekezaji na wafanyabiashara kushiriki kwa wingi katika kikao hicho.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.