Mkuu wa Mkoa wa Pwani mhe Abubakar Kunenge leo Agosti 6,2022 ameshiriki na Mhe Liberata Mulamula Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki katika Hafla ya utiaji Saini kwa Mkataba wa Uzalishaji wa Mbolea na Viuatilifu hai katika Kiwanda cha kuzalisha Bidhaa za Kibiolojia Tanzania (Tanzania Biotech Product Ltd) Kilichopo Kwenye Eneo la Viwanda TAMCO.
Hafla hiyo imeshuhudiwa pia na Mwakilishi wa Balozi wa Cuba Nchini Bw. Olando Dias Lodrick Naibu Waziri Viwanda, Biashara na Uwekezaji na Viongozi wa Wizara kutoka TAMISEMI Wizara ya Fedha na Management ya shirika la NDC.
Akitoa Salam za Mkoa Kunenge Amemshukuru Mhe Rais kwa kuboresha Mazingira ya Uwekezaji Mkoa wa Pwani
Ameeleza wanaendelea na jitihada za kuhakisha wanaongeza Viwanda katika Mkoa huo.
"Mkakati wetu ni wa aina mbili ikiwemo kukuza viwanda Vidogo na vya kati kuwa Viwanda Vikubwa na kupata Wawekezaji wapya wa Viwanda vikubwa" Ameeleza Kunenge.
Ameeleza kuwa Mkoa una Kongani 23 za Viwanda ikiwemo hiyo ya Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC). Ameeleza kuwa Kutokana na Jitihada kubwa za Mhe Rais Mkoa una Kongani ya Viwanda Kubwa Barani Afirika Kibaha -Kwala Sino Tan Kwala Industrial Park itakayo kuwa na Viwanda 350.
Amemshukuru Mhe Rais kwa kutoa kipaumbele kwenye Upatikanaji wa Miundombinu ya Umeme maji na Barabara kwa Mkoa huo. Miundombinu hii ni Muhimu kwa Uwekezaji.
"Muda si mrefu tutanza kunufaika na umeme kutoka Rufiji, Ujenzi kituo Cha Kupoozea Umeme unaendelea Chalinze kwa gharama ya Sh Bilioni 29.8 na ifikapo January 2023 tutaanza kupata Mw 1000 kutoka hapo" Ameeleza Kunenge.
Ameeleza kuwa Serikali inaendelea na Ujenzi wa Vituo vipya vya Kupoozea Umeme ambapo Tayari Wakazi wa Mkoa huo wameanza kunufaika ikiwemo kituo cha Luguruni MVa 180 kilichojengwa kwa gharama ya Sh Bilion15.2, Ujenzi wa Kituo Mkuranga cha MVA 240 kwa Gharama ya Sh Bilioni 59 na Ujenzi wa Kituo cha Zegereni MVA 240 kwa Gharama ya Tsh Bilioni 25
Ameeleza hali ya Upatikanaji wa Maji ni nzuri ambapo Serikali imetenga fedha kwa DAWASA kwa mwaka 2022/23 Sh. Bilion 175 kutekeleza Miradi mbalimbali na RUWASA kwa Mwaka huu wametengewa bilion 21.5.
Ameeleza kuwa Kutokana na kupatikana kwa Miundombinu muhimu ya Uwekezaji ikiwemo Sera nzuri Mkoa Pwani ni Mahali sahihi kwa Uwekezaji
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.